Na tukampa Musa Kitabu, na tukakifanya uwongofu kwa Wana wa Israili. (Tukawambia): Msiwe na mtegemewa ila Mimi! 1
Tafsir
Tabaka
Mafunzo
Tafakari
Majibu
Qiraat
Hadith
Na kama Mwenyezi Mungu Alivyomtukuza Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, kwa kumpeleka safari hiyo ya usiku, Alimtukuza Mūsā, amani imshukiye, kwa kumpa Taurati na Akaifanya ni yenye kuufafanua ukweli na kuwaongoza Wana wa Isrāīl na Akaifanya ni yenye kukusanya makatazo kwao ya kumfanya asiyekuwa Mwenyezi Mungu kuwa ni mtegemewa au ni muabudiwa wakawa wamtegemezea mambo yao.